Kwa mujibu wa tovuti ya Palestine info, mashirika hayo yalitoa taarifa hapo jana Jumanne yakisisitiza kwamba ulegezaji utawala huo mzingiro huo haujakuwa na athari yoyote katika kupunguza machungu na matatizo ya kimaisha ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Mashirika hayo ambayo yanajumuisha pia Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International na Shirika la Norway la Kutetea Wakimbizi yametangaza kwamba utawala haramu wa Israel pia unazuia kuingizwa katika Ukanda wa Gaza bidhaa muhimu za ujenzi.
Yamesema ulegezwaji wa mzingiro wa Gaza umesaidia tu katika kurahisisha utembeaji wa raia wa Gaza lakini kwamba ungali unazuia kuingizwa katika ukanda huo bidhaa muhimu za misaada ya kibinadamu. 704653