IQNA

Mashindano ya Qurani ya wanachuo huimarisha thamani za Qurani

22:04 - December 01, 2010
Habari ID: 2040818
Qari wa Qurani kutoka Libya amesema mashindano ya Kimataifa ya Qurani hasa ya wanafunzi wa vyuo vikuu huwa na nafasi muhimu katika kuimarisha utamaduni wa Kiislamu na thamani za Qurani.
Hayo ni kwa mujibu wa Badrudin Abdul Hakim Al Warfawi, mwakilishi wa Libya katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa Ajili ya Wanachuo Waislamu. Qari huyo wa Misri amesema kuwa mashindano kama hayo ya Qurani vile vile yana mchango mkubwa katika kuimarisha uhusiano miongoni mwa nchi za Kiislamu.
Akizungumza na IQNA amesema kuwa: “Nimeshiriki katika mashindano ya Qurani nchini Libya na kushinda zawadi kadhaa. Baada ya kuibuka mshindi katika mashindano yaliyopita, nimeamua kushiriki katika mashindano ya kimataifa nchini Iran”
Al Warfawi ameashiria harakati za Qurani nchini Libya na kusema: “Kila mwaka Libya huandaa mashindano ya kimataifa ya Qurani ambayo huwa na washiriki kutoka nchi za Kiislamu ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran”.
704405
captcha