Kipindi hicho cha televisheni kinaonyeshwa kwa shabaha ya kuarifisha tukio la Ashuraa na kuuawa shahidi Imam Hussein (as) na masahaba zake.
Mpango wa televisheni ya serikali ya Uturuki ya TRT wa kuarifisha tukio la Ahuraa ulianza mwaka 2007 kwa kuonyesha kipindi maalumu kuhusu matukio ya Karbala kilichopewa jina la 'Mahala Pote ni Karbala'. Vipindi hicho mbali na kuarifisha Ahlul Bait wa Mtume Muhammad (saw), vinabainisha sababu za uadui wa Bani Umayyah dhidi ya Imam Ali bin Abi Twalib (as), sababu za suluhu na mapatano ya Imam Hassan (as) na Muawiyah bin Abi Sufian, mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala, itikadi ya Imam wa Zama (as) na umuhimu wa tukio la Ashuraa. 704601