Kikao cha pili cha utafiti wa Qur'ani wa Imam Mussa
Kikao cha pili cha mijadala ya kitaalamu kuhusu utafiti wa Qur'ani wa Imam Mussa Sadr kimepangwa kufanyika kesho Jumatatu katika makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA mjini Tehran.
Kikao hicho kinasimamiwa na shirika la IQNA likishirikiana na Taasisi ya Utamaduni na Uhakiki ya Imam Mussa Sadr.
Kikao hicho kitahutubiwa na Dakta Ghulamreza Zakiani, mwanachama wa jopo la elimu la Chuo Kikuu cha Allamah Tabatabai.
Kikao hicho pia kitahudhuriwa na binti ya Imam Sadr Haura Sadr. Watu mbalimbali wanakaribishwa kuhudhuria kikao hicho. 706661