Hayo yamesemwa na Muhammad Niyazi, karii na mwakilishi wa Misri katika mashindano ya kimataifa ya wanachuo wa Kiislamu. Amesema kuwa kamati inayosimamia mashindano hayo imeyatangaza vyema kwa kadiri kwamba washiriki hawakupata matatizo yoyote kuhusu mashindano yenyewe yatakavyofanyika, wakati na mahala pake.
Muhammad Niyazi amesema kuwa mashindano hayo ya kimataifa ya wanachuo Waislamu yanatayarisha uwanja mzuri kwa ajili ya kubadilishana mawazo na mitazamo wanachuo wa Kiislamu. Vilevile yanawapa fursa ya kujadili matatizo ya nchi za Kiislamu.
Katika upande mwingine karii huyo mwenye umri wa miaka 18 anasema kuwa alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa mtoto mdogo akisaidiwa na baba yake mzazi na kwamba anafadhilisha kiraa ya Sheikh Mustafa Ismail.
Amesema kuwa hadi sasa ameshiriki katika mashindano mengi ya Qur'ani na kutunukiwa zawadi nyingi. Muhammad Niyazi amesema kuwa kuhifadhi Qur'ani kunahitaji subira na uvumilivu na anaamini kuwa ni rahisi kuhifadhi Qur'ani katika kipindi cha utotoni kwani katika kipindi hicho mtoto mdogo huwa na uwezo wa kushika kifuani yale anayofundishwa. 705933