Nuskha hiyo yenye uzito wa kilo 10 na upana wa sentimita 15 kwa 35 kwa 45. Aya zake zimechongwa katika kurasa za mbao ya mbinu kadhaa za uandishi hati za Kiarabu ikiwa ni pamoja na Naskh, Sols, and Nasta’liq.
Mohsen Fuladi aliyetayarisha nuskha hii ya kipekee ya Qur'ani anasema alianza kazi yake mwaka 2005 kwa mnasaba wa siku ya Milad un Nabi SAW. Amesema alikuwa akifanya kazi kwa masaa 12 kwa siku.
Hafla ya kuzinduliwa nuskha hiyo ya Qurani imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Hujjatul Islam Hamid Mohammadi ambaye anasimamia masuala ya Qurani katika wizara hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo amesema Wizara ya Utamaduni inasisitiza juu ya utumiaji wa mbinu za sanaa katika kueneza mafundisho ya Qur'ani.
706411