IQNA

Vitabu vya Iran katika maonyesho ya vitabu Tanzania

15:59 - December 06, 2010
Habari ID: 2043247
Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Dar-es-Salaam imeshiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu nchini Tanzania na kuwasilisha bidhaa za utamaduni kutoka Iran kama vitabu, CD/DVD na majarida.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Vitabu nchini Tanzania yalifanyika katika Ukumbi wa Ubunge kuanzia Novemba 25 na kuendelea kwa siku tano.
Sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo zilihuduriwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vitabu Tanzania (Bamvita), Walter Bgoya kati ya wageni wengine. Maonyesho hayo yalishirikisha taasisi 25 za uchapishaji nchini Tanzania na vilevile kutoka nchi za mashariki na kusini mwa Afrika.
707412
captcha