Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, Abdul Raouf bin Rajab, Msemaji wa OIC ameongeza kuwa: "Jumuiya ya Nchi za Kiislamu inafanya bidii kuhakikisha kuwa taswira sahihi ya Uislamu kuhusu masuala kama vile maelewano, kustahamiliana, amani na kuheshimu dini na tamaduni mbalimbali inaakisiwa ipaswavyo'.
Amesema chuki dhidi ya Uislamu ni jambo ambalo litaathiri vibaya amani na utulivu duniani. Amesema jamii ya kimataifa ina wasiwasi kuhusu kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu na kuongeza kuwa: "Jumuiya ya Nchi za Kiislamu imepanga warsha katika mji mkuu wa Poland, Warsaw kuanzia Disemba 8-10 kwa lengo la kujadili hali ya jamii za Waislamu katika maeneo ya kati na magharibi mwa bara Ulaya"
707464