Kwa mujibu wa tovuti ya IQNA kongamano hilo limeandaliwa na Baraza Kuu la Kiislamu la Misri na litawashirikisha wasomi pamoja na mawaziri wa wakfu kutoka nchi za Kiislamu na vilevile jumuiya za Kiislamu kutoka zaidi ya nchi 100 duniani.
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri Bw. Mahmoud Hamdi Zakzuk amesema kongamano hilo la siku nne litajadili nafasi ya Quds katika dini na historia na wadhifa wa Waislamu na Waarabu katika kuhami mji huo mtakatifu unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha amesema kuzima njama za utawala wa Kizayuni za kuuyahudisha mji wa Quds ni kati ya masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho.
Washiriki katika kongamano hilo wanatazamiwa kutafuta njia za kuimarisha umoja miongoni mwa nchi za Kiislamu kuhusu kadhia ya Quds.
707533