Gazeti la nchi hiyo la al-Watan limeandika kwamba mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Huduma za Qur'ani ya Bahrain. Licha ya kuhifadhi Qur'ani mashindano hayo pia yatahusu nyanja nyinginezo zinazohusiana na kitabu hicho kitakatifu.
Mashindano hayo yatamalizika hii leo Jumanne na sherehe ya kuyafunga kufanyika hapo kesho Jumatano badaa ya kuswaliwa swala za Maghrib na Ishaa. Wawakilishi kutoka nchi za Bahrain, Kuwait, Imarati, Saudi Arabia, Libya, Bangladesh, Oman, Ugiriki, Morocco, Tajikistan, Qatar, Sudan, Chad, Iraq, Yemen, Jordan, Syria, Palestina, Lebanon na Pakistan wanashiriki katika mashindano hayo. 708092