Kaptain Mehdi Meydani Naibu Mkuu wa Kituo cha Darul Qur'an katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mashindano hayo yatawahusisha wanajeshi na makurutu.
Amesema washiriki watashindana katika viwango vya tajwid, tarteel, tafsiri, ufahamu wa Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani na Adhana.
Mashindano hayo ya siku nne yatawakutanisha pamoja walioshiriki katika mchujo kote nchini katika vikosi vya jeshi la nchi kavu, jeshi la wanamaji na jeshi la anga.
Sherehe za ufunguzi zitafanyika Disemba 20 na kuhudhuriwa na makamanda wa jeshi na baadhi ya viongozi wa kiraia.
Washindi wa mashindano hayo watashiriki katika mashindano ya kitaifa ya vikosi vyote vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyopangwa kufanyika Mei 2011.
708159