Maudhui ya kikao hicho ilikuwa aya ya 20 ya surah Adh-Dhariyat- inayosema: "Na katika ardhi zipo ishara kwa wenye yakini."
Kongamano hilo limetayarishwa na Jumuiya ya Kuilinda Qur'ani Tukufu.
Zaqul Najjar mwanazuoni maarufu wa Jordan na mtaalamu wa miujiza ya Qur'ani alikuwa kati ya wazungumzaji katika kongamano hilo. Aliashiria aya ya 25 ya Suratul Hadid isemayo: "Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda".
Zaqul Najjar amesisitiza kuhusu nukta ya kimuujiza ya aya hii ya Qur'ani Tukufu.
Aidha Abdul Qadir Abid mwanajilojia wa Chuo Kikuu cha Jordan naye amewasilisha makala kuhusu miujiza ya Qur'ani kuhusu maji.
709958