Mwenyekiti wa baraza la mji huo Hamid Shabab amesema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kutoa sura mpya ya mpango wa miji dada ya Fas na Quds na vilevile kutekeleza ratiba mbalimbali za kupanua na kustawisha utamaduni wa Quds Tukufu.
Vilevile amepongeza juhudi za Mfalme Muhammad wa Sita wa Morocco za kulinda historia, utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu wa mji wa Quds huko Palestina na kukabiliana na njama za kutaka kuuyahudisha mji huo wa Kiislamu. 710296