IQNA

Kongamano la Kimataifa la Shule za Qur'ani kufanyika Imarati

18:05 - December 11, 2010
Habari ID: 2046073
Kongamano la Kimataifa la Shule za Qur'ani limepangwa kufanyika mapema mwezi Februari mwakani likisimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Khoja Shia Ithnaasharia katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kituo cha habari cha 'Shia974' kimeripoti kuwa kongamano hilo litafanyika kwa lengo la kubainisha mitazamo ya pamoja kuhusu shule za Qur'ani, njia za kutekeleza mitazamo hiyo, kubadilishana habari na uzoefu kati ya wataalamu wa elimu na kuanzisha kanali katika sherehe itakayohudhuriwa na wataalamu na wafuatiliaji wa masuala ya kidini na kijamii.
Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Khoja Shia Ithnaasharia Sayyid Ali Reza Taqawi amewataka wazazi, walimu wa shule za Qur'ani na za Kiislamu, wanafunzi wa shule hizo na wahubiri wa Kiislamu kurejea katika mtandao wa intaneti wa www.surveymonkey.com na kujaza fomu makhsusi. Muda wa mwisho wa kutuma fomu hizo ni tarehe 20 Disemba.
Amesema kuwa majibu ya fomu hizo yatajadiliwa na wataalamu katika Kongamano la Kimataifa la Shule za Qur'ani nchini Imarati na kutumiwa na wataalamu kwa ajili ya kuboresha hali ya shule za Kiislamu.
Makao makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Khoja Shia Ithnaasharia yako nchini Pakistan. 710650


captcha