IQNA

Wanaohifadhi Qur'ani wanapaswa kuwa vigezo vya kimaadili

16:36 - December 13, 2010
Habari ID: 2047494
Wanaohifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu wanapswa kuwa vigezo vya kimaadili katika jamii wanamoishi.
Kwa mujibu wa Sinaudin Tatarevic hafidh wa Qur'ani kutoka Bosnia Herzegovina amesema anajitahidi kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yake na anawasaidia marafiki zake kuufahamu vyema Uislamu.
Tatarevic ambaye atawakilisha Bosnia Herzegovina katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu nchini Iran ameongeza kuwa, hafidh wa Qur'ani anapaswa kutumia ujuzi wake wa Qur'ani katika maisha yake ya kila siku.
Kuhusu kushiriki kwake katika mashindano mbalimbali ya Qur'ani, amesema alihudhuria mashindano ya kiraa nchini Misri katika mwezi wa Ramadhani na vilevile Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Bara Ulaya yaliyofanyika Croatia ambapo alipata nafasi ya sita.
Kuhusu Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yatakayofanyika Iran ametoa wito kwa waandalizi kuongeza kitengo cha tafsiri. Amesisitiza kuwa hafla za kimataifa za Qur'ani ni nafasi muafaka ya kustawisha Umoja wa Kiislamu.
Tatarevi ambaye anasoma lugha ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Sarajevo ameashiria juhudi zake za kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kusema: "Nilianza kuhifadhi Qur'ani nilipokuwa kidato cha tatu katika shule ya upili. Kila siku nilikuwa nikihifadhi kurasa mbili za Qur'ani na baada ya mwaka moja nilifanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima".
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanachuo Waislamu yatafanyika Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran kuanzia Januari 9-11.
709929
captcha