Mkuu wa Shirika la Mashahidi Hujjatul Islam Khalili amesema kuwa hatua hiyo inalenga kueneza fikra za Qur'ani na kuimarisha ujumbe wa Qur'ani katika jamii.
Amesema moja ya njia bora za kujifunza Qur'ani na kuwa na uwezo wa kufasiri aya za kitabu hicho ipasavyo ni kukariri. 'Flash Kadi' zilizosambazwa zina uwezo wa kukariri maneno mara kadhaa na hivyo kurahisisha ufahamu wa Qur'ani Tukufu'. Ameongeza kuwa mashindano ya Qur'ani kwa mujibu wa mpangilio wa 'flash kadi' hizo yataandaliwa na Kituo cha Qur'ani cha Shirika la Mashahidi katika sherehe za wiki ya "Alfajiri 10" ambayo hufanyika mwezi Februari kila mwaka kwa mnasaba wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 711854