Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, kikao hicho kinafanyika kwa ushirikiano wa shirika hilo kwa madhumuni ya kuimarisha mwamko wa washiriki kuhuisiana na umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya tamaduni na dini tofauti na pia kutafuta ufumbuzi wa kuboreshwa thamani za kiutu zikiwemo za amani na uadilifu. Kuimarishwa ushirikiano kati ya nchi wanachama wa ISESCO kuhusiana na suala hilo pia ni miongoni mwa malengo ya kufanyika kikao hicho.
Kikao hicho kimepangwa kumalizika hapo kesho Jumatano. 712409