IQNA

Warsha ya kwanza ya kimataifa ya Qurani Tukufu nchini Kuwait

12:53 - December 18, 2010
Habari ID: 2048584
Warsha ya kwanza ya kimataifa ya Qur'ani yenye anuani ya ‘Mafundisho na Hifdhi ya Qur'ani’ itafanyika nchini Kuwait chini ya kauli mbiu ya ‘kushirikiana katika kuhudumia Qur'ani’.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Anbaa, Adel al Fallah Naibu Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait amesema kuwa, ‘warsha hiyo itafanyika Jumatatu Disemba 20 katika Msikiti Mkuu na itasimamiwa na Idara ya Masuala ya Qur'ani’.
Mbali na wataalamu wa Qur'ani kutoka Kuwait, warsha hiyo pia itawashirikisha pia wasomaji na wanaohifadhi Qur'ani kutoka nchi mbalimbali, wasomi wa sayansi za Qur'ani na vilevile wanafunzi bingwa wa hifdhi na tajweed.
Adel al Fallah ameongeza kuwa kamati na taasisi kadhaa za Qur'ani nchini Kuwait zimetoa ushirikiano wao katika kufanikisha warsha hiyo.
713221
captcha