IQNA

Kikao cha kusoma Qur'ani chafanyika Siku ya Ashura

13:07 - December 18, 2010
Habari ID: 2048585
Kikao cha kusoma Qur'ani Tukufu kilifanyika Jumatano usiku hadi Alhamisi asubuhi (Siku ya Ashura) katika Msikiti wa Al Mahdi mjini Rey kusini mwa Tehran.
Hafla hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wa Mji wa Rey na ilihudhuriwa na idadi kuwa ya waumini waliokuwa wanaomboleza kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS.
Makarii wa kimataifa kutoka mji wa Rey walishiriki katika hafla hiyo ambayo iliwavutia sana hadhirina.
Aidha kulisomwa mashairi kwa mnasaba wa Ashura ambayo ni siku ya Waislamu kukumbuka kwa majonzi tukio la kuuawa shahidi Imam Hussein AS akiwa pamoja na masahaba wake watiifu takribani miaka 1400 iliyopita katika jangwa ya Karbala.
Hafla hiyo pia ilikuwa na mawaidha ambapo wazungumzaji walifafanua harakati ya Ashura na malengo yake matakatifu.
713207
captcha