Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa Russia amezungumzia uwezekano mkubwa wa kujengwa msikiti mpya katika mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ria Novosti, Putin ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha kila mwaka cha majibu na maswali mbele ya waandishi habari amesema kuwa tayari mipango ya ujenzi wa msikiti huo imekamilika na kuwa ujenzi huo utaanza hivi karibuni.
Msikiti huo utajengwa katika eneo la kusini mashariki mwa Moscow ambalo wakaazi wake wengi ni Waislamu.
Maafisa wa serikali wa eneo hilo wamesema kuwa kabla ya kuchukuliwa uamuzi wa kujenga msikiti huo, majadiliano na mashauriano yalifanyika kati yao na wakaazi wasio Waislamu wa eneo hilo.
Hivi sasa Moscow ina misikiti minne pekee ambapo kila mmoja una uwezo wa kupokea watu 500. 713253