Kituo cha habari cha Europe1 kimeripoti kuwa msikiti huo una minara miwili yenye urefu wa mita 50 na umejengwa katika ghorofa tatu. Ghorofa ya kwanza inatumiwa kwa ajili ya ibada ya swala ya wanaume, ghorofa ya pili inatumiwa na wanawake na ya tatu inatumiwa kwa ajili ya kutoa masomo ya Kiislamu na maktaba ya msikiti huo.
Ujenzi wa msikiti huo ulianza mwaka 2003 katika mji wa Rotterdam na ilitazamiwa kuwa ungekamilika katika kipindi cha miaka mwili. Hata hivyo mradi huo ulichelewa kutokana na vizuizi na matatizo yaliyosababishwa na vyama na makundi yanayoupiga vita Uislamu nchini Uholanzi.
Msikiti huo na kituo chake cha Kiislamu unaweza kupokea watu elfu tatu na kwa msingi huo unahesabiwa kuwa msikiti mkubwa zaidi katika Ulaya magharibi. 713614