Wakati wimbi la hasira na malalamiko ya Waislamu kote duniani dhidi ya vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu likiwa bado halijatulia, kasisi mmoja wa Kikopti wa Misri ametengeneza filamu mpya na kuirusha katika mtandao wa Kikristo.
Filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu imezijeruhi mno hisia na nyoyo za Waislamu wa Misri.
Filamu hiyo iliyojaa hisia za kibaguzi, inautuhumu Uislamu kuwa ni dini ya kikatili na kwamba Waislamu ni watu wenye kiu ya kunywa damu za watu.!
Kasisi Markos Aziz wa kanisa la Kikopti la Misri ambaye ndiye aliyetayarisha filamu hiyo ameonyesha dharau kubwa mwanzoni mwa filamu hiyo na kutangaza kuwa amewatunuku Waislamu zawadi hiyo kwa mnasaba wa mwaka mpya wa Miladia.
Filamu hiyo ambao kwa sasa inaonyeshwa kwenye mtandao wa Wakristo wa Kikopti wa Misri, ni mjumuiko wa filamu kadhaa zilizotengenezwa na kuonyeshwa na Wamagharibi huko nyuma.
Filamu hiyo pia inajumuisha sehemu ya filamu ya Fitna iliyotengenezwa ana mbunge mkorofi na mbaguzi wa Uholanzi Geert Wilders. 713795