Kikao hicho kilichoandaliwa na Baraza la Waislamu wa Morocco Wanaoishi Ulaya' kimefanyika kwa ushirikiano wa Muungano wa Vituo vya Kiislamu na Kiutamaduni wa Catalonia. Kimehudhuriwa na wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu, maafisa wa serikali ya Catalonia na idadi kadhaa ya wahadhiri wa vyuo vikuu vya bara Ulaya.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Taher Tijkani, mkuu wa baraza lililotajwa amesema kuwa wameandaa kikao hicho kutokana na udharura wa kufanyika mazungumzo kati ya ulimwengu wa Kiislamu na wa Magharibi. Amesema kikao hicho kimejadili umuhimu wa kutekelezwa sheria za Kiislamu barani Ulaya kwa kutilia maanani thamani za bara hilo.
Amesema katika mtazamo huo wana lengo la kuimarisha mazungumzo kati ya tamaduni mbili hizo muhimu za dunia.
Taher Tijkani amesema nafasi muhimu ya viongozi wa kidini haipasi kupuuzwa kuhusu jambo hilo kwa sababu wana fikra na maoni yao yana umuhimu mkubwa katika kushajiisha hisia za kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti. 714690