Kwa mujibu wa idara ya habari ya uhusiano wa kimataifa katika Shirika la Awqaf, Hujjatul Islam Muhammad Ali Raghebi amesema kuna vitivo 14 vya sayansi za Qur'ani nchini Iran ambapo kuna wanachuo 3000 katika shahada ya kwanza (BA) na shahada ya uzamili (M.A).
"Watakaofuzu katika shahada ya uzamivu watajiunga na mabaraza ya kisayansi ya vitivo hivyo", ameongeza Sheikh Ali Raghebi.
Aidha amesema kuwa nchini Iran athari za Qur'ani zinabainika katika mazungumzo na tabia za wananchi. Vilevile amesema washindi wa mashindano ya Qur'ani wanaweza kusajiliwa katika vitivo vya sayansi za Qur'ani bila kufanya mitihani.
714601