Kikao hicho cha kimataifa ambacho kitafanyika tarehe 22 Disemba kitaendelea kwa siku mbili na kuhutubiwa ya Ayatullah Muhammad Ali Tas-khiri, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu na wanazuoni wengine wa ulimwengu wa Kiislamu.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu imesema kuwa kikao hicho kitafanyika katika tarehe iliyotajwa katika mji mkuu wa Jordan.
Kikao hicho ambacho kitafanyika kwa mwaliko wa Katibu Mkuu wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO kitajadili masuala kama 'misingi ya kinadharia ya ijtihadi na usasa na taathira za ijtihadi na usasa katika ustawi wa utamaduni wa jamii za Kiislamu na kadhalika.'
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Ali Tas-khiri atahutubia kikao hicho akizungumzia maudhui ya ijtihadi na taathira zake katika mageuzi ya kiutamaduni. 715278