Ihsanoglu amesema katika ujumbe huo kwamba japokuwa wanawake wamekuwa wahanga wa ada, itikadi na mitazamo isiyokuwa sahihi katika jamii lakini Uislamu umemlinda na kumpa hadhi mwanamke na kumhamasisha kwa ajili ya kushiriki katika nyanja mbalimbali za jamii.
Amesisitiza kwamba Qur'ani na suna za Mtume (saw) zinatoa mafundisho ya kukirimu na kuheshimiwa wanawake na kusisitiza juu ya umuhimu wao katika jamii bega kwa bega na wanaume.
Ihsanoglu amesema katika hali ya sasa kunashuhudia maendeleo makubwa ya wanawake wa Kiislamu na kushinda vizingiti na matatizo mbalimbali japokuwa wanakabiliwa na matatizo mengi. Amesema hata hivyo wanawake wa Kiislamu wanaendeleza juhud za kuwa na naasi kubwa katika masuala ya kijamii kama kuchukua maamuzi muhimu, kupunguza umaskini, medani za elimu mazungumzo kati ya tamaduni, haki za binadamu na suala la kuimarisha amani na usalama.
Amesema kuwa mkutano wa tat wa mawaziri wa nchi za Kiislau unaojadili nafasi na mchango wa wanawake katika jamii za Kiislamu ni hatua kubwa ya maendeleo ya wanawake wa Kiislamu. 715197