IQNA

Iran yateua wawakilishi katika mashindano ya Qurani ya wanachuo

12:45 - December 21, 2010
Habari ID: 2050713
Mohammat Khatib na Hamed Valizadeh watawakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa ajili ya wanachuo Waislamu.
Khatibu atashiriki katika kiwango cha hifdhi naye Valizadeh ataiwakilisha Iran katika kiwango cha qiraa.
Wawili hao wamechaguliwa Desemba 20 baada ya kushiriki katika fainali ya mchuko iliyowashiriisha Abuzar Karami (hifdhi) na Majid Faqih (qiraa).
Mashindano hayo ya mchujo yalifanyika katika Taasisi ya Harakati za Qurani ya Wanachuo wa Iran. Wasimamizi wa mchujo huo walikuwa mabingwa wa Qurani nchini Iran ambao ni Rahim Khaki, Mahdu Qarasheikhlu, Amri Aghayi, Sayyed Ali Sarabi na Ahmad Abukqasimi.

Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa ajili ya wanachuo Waislamu yatafanyika Januari 9-11 katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran ambapo maqari na mahafidh wa Qurani kutoka zaidi ya nchi 40 watashiriki.
captcha