IQNA

Wanafunzi 40 elfu wajifunza Qurani mkoani Mazandaran Iran

12:45 - December 21, 2010
Habari ID: 2050714
Zaidi ya wanafunzi 40 elfu wanapata mafunzo katika shule 1001 za Qurani mkoani Mazandaran kaskazini mwa Iran.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Darul Quran ya Wizara ya Elimu mkoani humo wanafunzi hao watapata masomo ya kawaida kwa miezi tisa na baadaye kujiunga na taasisi maalumu za Darul Quran.
Mkuu wa Darul Quran katika mkoa wa Mazandaran Hussein Qurbani anasema kuwa juhudi zinafanyika kuwavutia wanafunzi zaidi katika masomo ya Qurani ili kuimarisha ufahamu wao wa kitabu hicho kitakatifu.
Amesema idadi ya darasa za Qurani zinatazamiwa kuongezeka mkoani humo kwa himaya ya idara ya elimu.
715083
captcha