IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Wastani wa Kiislamu' chafanyika Yemen

16:48 - December 21, 2010
Habari ID: 2051185
Kikao cha kimataifa cha 'Wastani wa Kiislamu' kimeanza leo Jumanne katika mji wa Tarim nchini Yemen.
Kikao hicho cha siku tatu kinafanyika katika mji wa Tarim kufuatia mji huo kuchaguliwa kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2010.
Abu Bakr Ali al-Mash'huri, mkuu wa kamati inayosimamia kikao hicho amesema kuwa wanafikra na wasomi mashuhuri wa Kiislamu akiwemo Ali Juma, Mufti wa Misri na Fuad Hahdi mhubiri wa Saudi Arabia wanashiriki katika kikao hicho.
Amesema kubainishwa msimamo wa wastani wa mafundisho na maadili ya Kiislamu, nafasi ya Tarim katika kuimarisha uhubiri wa Kiislamu, mchango wa Hadhramaut katika kuimarisha umoja wa kijamii baina ya Waislamu na kuenezwa amani ulimwengu ni miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kongamano hilo. 715488
captcha