Tovuti ya Ummid imeripoti kuwa wasomaji wa Qur'ani Tukufu kutoka India na nchi nyingine za dunia zikiwemo Iran, Pakistan, Uingereza na Panama watashiriki katika mashindano hayo.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Zinat al-Qur'an yataendelea kwa muda wa siku mbili. Washindi wa kwanza hadi nne watatunukiwa zawadi nono ya fedha na washiriki wengine wote kuzawadiwa loho ya shukrani na ukumbusho. 715813