IQNA

Kongamano la 'Ustaarabu wa Kiislamu' kufanyika Pakistan

18:41 - December 22, 2010
Habari ID: 2051832
Kongamano la Kimataifa la 'Ustaarabu wa Kiislamu; Uwezo na Changamoto' ambalo lilikuwa lifanyike Novemba mjini Lahore Pakistan sasa litafanyika mwezi Machi mwakani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Chuo Kikuu cha Menejmenti na Teknolojia cha Lahore UMT, kongamano hilo litafanyika kwa usimamizi wa kitivo cha Sayansi za Jamii chuoni UMT kuanzia 9-10 Machi.
Kati ya masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na 'nafasi na ustawi wa ustaarbu wa Kiisamu, 'sifa za ustaarabu wa Kiislamu na athari zake kwa staarabu zingine kubwa duniani', 'umoja wa anuai katika ustaarabu wa Kiislamu', 'nafasi ya ustaarabu wa Kiislamu katika fikra za kidini, sayansi za kijamii na kimaumbile na uhusiano wa kimataifa, sanaa, utamaduni, usanifu majengo na sheria'.
Makala katika kongamano hilo zitakuwa kwa lugha Kiingereza na Kiarabu. 716789

captcha