Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, washiriki wa kongamano hilo wamependekeza kuwa maktaba ziwe na nafasi muhimu katika kuimarisha utafiti wa kisayansi, mafunzo na ustawishaji ujuzi wa sayansi za kompyuta miongoni mwa wanachuo na wahadhiri.
Aidha kumetolewa wito wa kuimarishwa uandishi wa vitabu na ubadilishanaji wa vitabu vya kale na nadra.
Kongamano la Kwanza la Wakuu wa Maktaba za Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu lilifanyika chini ya anuani ya: "Kuelekea kwenye Muungano wa Kistratijia wa Kujenga Jamii Zenye Elimu".
Karibu wakuu 125 wa maktaba za vyuo vikuu vya nchi za Kiislamu walishiriki katika kongamano hilo.
716651