IQNA

India, mwenyeji wa kongamano kubwa la Waislamu duniani

13:05 - December 23, 2010
Habari ID: 2052035
Moja ya makongamano makubwa zaidi ya Waislamu au kwa ibara nyingine ijtimai ya Waislamu duniani, linatarajiwa kufanyika tokea Jumamosi tarehe 25 hadi Jumatatu tarehe 27 Disemba.
Kongamano hilo ambalo linawajumuisha watu laki 700 limepangwa kufanyika katika mji wa Bhopal. Kwa mujibu wa tovuti ya Deccan Herald kongamano hilo huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Wahubiri wa India kwa lengo la kueneza Uislamu, kuwashajiisha Waislamu wafanye mambo mema, wajiepushe na dhambi, kumfahamu zaidi Mwenyezi Mungu na kufuata njia ya Mtume Mtukufu (saw). Kufikia sasa tayari misafara ya Waislamu kutoka Russia, Cambodia, Thailand, Indonesia, Malaysia na Sri Lanka imekwishawasili nchini India kushiriki katika ijtimai hiyo. Misafara mingine ya Waislamu kutoka katika zaidi ya nchi 30 za dunia zikiwemo Australia, Uingereza na Afrika Kusini inatazamiwa kujiunga na misafara hiyo iliyokwishawasili India.
Askari 1200 wametumwa katika sehemu inayofanyika ijtimai hiyo ili kulinda amani na usalama wa washiriki. Waandaaji wa ijtimai hiyo pia wameweka utaratibu maalumu wa kuwasaidia watu dhaifu kimwili, kuweza kushiriki na kunufaika na ijtimai hiyo.
Ijtimai ya Waislamu nchini India ilianza kutekelezwa mwaka 1974 sambamba na kutangazwa uhuru wa nchi hiyo na hadi sasa imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mji wa Bhopal. Tokea wakati huo hadi kufikia mwaka 2001 ijtimai hiyo ilikuwa ikifanyika katika Msikiti wa Taj al-Masjid ambao ni moja ya misikiti mikubwa barani Asia, lakini baada ya hapo imekuwa ikifanyika katika eneo la Itkhori mjini humo.
Kwa kuwa na Waislamu milioni 140, India ni nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani baada ya Indonesia na Pakistan. 716876
captcha