Ripoti hiyo inabainisha kwa kina baadhi ya athari mbaya za mzingiro huo dhidi ya wakazi madhlumu wa Ukanda wa Gaza na kuendelea upuuzaji wa utawala wa Kizayuni dhidi ya matakwa ya walimwengu kuhusiana na udharura wa kuondolewa mzingiro huo.
Uvamizi wa Wazayuni katika Ukanda wa Gaza ulimalizika mwaka 2004 lakini tokea wakati huo hadi sasa ukanda huo umekuwa chini ya mzingiro mkubwa wa utawala haramu wa Israel.
Mzingiro huo ulizidishwa mwaka 2007 ambapo mawasiliano ya karibu watu milioni 1.7 wanaoshi katika ukanda huo na ulimwengu wa nje yamekatwa kikamilifu. 717398