IQNA

Kiraa ya Qur'ani kupitia intaneti yahimizwa

12:48 - December 25, 2010
Habari ID: 2052665
Karii mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran amehimiza kuanzishwa mafunzo ya kiraa ya Qur'ani Tukufu kupitia intaneti kwa ajili ya wanafunzi wa kimataifa.
Ahmad Abulqasemi ambaye ni kati ya majaji wa Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani kwa ajili ya Wanachuo Waislamu amesema Jumuiya ya Harakati za Qur'ani ya Wanachuo Wairani (ambayo inaandaa mashindao hayo) inapaswa kuendelea kuwa na mawasiliano na washiriki baada ya mashindano hayo.
"Jumuiya hii pia inaweza kuwa na kozi za intaneti kwa ajili ya wanachuo kutoka nchi zinginezo ambao hawana fursa ya kuonana ana kwa ana na maustadhi bingwa wa Qur'ani", ameongeza. Amesema kozi kama hizo zinaweza kufanyika kila wiki ili kuwawezesha wanachuo kuimarisha ujuzi wao wa Qur'ani.
Amesema duru zilizopita za mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa ajili ya wanachuo Waislamu zilifana.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani kwa ajili ya Wanachuo Waislamu yatafanyika katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran kuanzia Januari 9-11 na kuwashirikisha wanachuo kutoka zaidi ya nchi 40. 716967
captcha