Ayatullah Imami Kashani amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa na kubainisha kwamba, daima maadui wamekuwa wakifanya njama za kueneza ufisadi katika jamii, kuuwa wasomi na kukabiliana na ustaarabu wa Kiislamu. Amesema kuwa, baada ya maadui kushindwa kuzuia utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu sasa wameamua kuchukua hatua ya kuuwa wasomi wa Kiislamu na kuzusha hitilafu za kimadhebu kwa kutekeleza mashambulio ya kigaidi kama yale yaliyowalenga waombolezaji wa Imam Hussein AS siku ya Taasua huku kusini mashariki mwa Iran. Ayatullah Kashani amebainisha sifa maalumu za ustaarabu wa Kiislamu na kusisitiza kwamba, mitazamo ya kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa ya Uislamu imepelekea mataifa mengi kuupokea Uislamu kama mwokozi baada kuwa katika mashinikizo na dhulma kwa miaka mingi. 717366