Mashindano hayo yanasimamiwa na Wizara ya Wakfu ya Masuala ya Kiislamu ua Saudi Arabia na yatafanyika kwa mara ya kwanza katika kumbi za Masjidul Haram.
Katibu wa mashindano hayo Mansour Muhammad al Samiih amesema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na kwamba washindani kutoka nchi mbalimbali duniani watashiriki katika mashindano hayo ya Qur'ani.
Amesema mashindano hayo ni hatua ya kuimarisha urafiki na udugu kati ya vijana wa nchi za Kiislamu wenye lugha na utaifa tofauti na kwamba malengo yake ni pamoja na kuhimiza zaidi juu ya umuhimu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, udharura wa kusoma, kufasiri Qur'ani na kuwahamasisha vijana Waislamu kuhifadhi na kutaamali aya za kitabu hicho.
Mashindano hayo ya kimataifa yanafanyika katika ngazi tano tofauti za hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tajwiidi na tafsiri, hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tilawa na tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 za Qur'ani pamoja na tilawa na tajwidi, hifdhi ya juzuu 10 pamoja na tilawa na tajwidi na hifdhi ya juzuu 5 za Qur'ani pamoja na tilawa na tajwidi makhsusi kwa wawakilishi wa nchi zisizokuwa za Kiislamu.
Washiriki 122 kutoka nchi 38 duniani na washiriki 66 kutoka jumuiya 26 za Kiislamu kutoka nchi zisizokuwa za Kiislamu wanashiriki katika mashindano hayo. 717617