IQNA

Kozi ya 'Qur'ani na Lugha ya Kiarabu' kufanyika Afrika Kusini

12:44 - December 26, 2010
Habari ID: 2053096
Kozi ya mafundisho ya masomo ya Qur'ani na lugha ya Kiarabu itafanyika Afrika Kusini kuanzia Januari 15 kwa himaya ya Taasisi ya Dar al-Mahamid katika mji wa Cape Town.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kozi hiyo ya msimu wa mapumziko itafanyika katika Msikiti wa Al Monawara mjini Cape Town.
Darul Mahamid imetangaza kuwa kozi hiyo itaanza mwaka 2011 na itajumuisha vijana wa kiume na kike walio na umri wa zaidi ya miaka 12.
Wakati huo huo Darul Mahamid imeandaa kambi maalumu kwa ajili ya vijana ili kuhakilisha kuwa hawapotei katika wakati wa mapumziko ya msimu wa joto Afrika Kusini. Kozi hizo zimeanza tarehe 17 Disemba na zitaendelea hadi Januari Mosi.
Vijana wanaoshiriki katika kambi hiyo wanapata mafundisho ya kiraa, Qasida, dhikr na lugha ya Kiarabu. Aidha kutakuwa na michezo mbalimbali kwa vijana.
717845

captcha