Kongamano hilo limefanyika kwa lengo la kubainisha sira na mwenendo wa maisha ya Nabii Muhammad (saw) kwa lengo la kumfuata mtukufu huyo na kupata saada na ufanisi.
Maulana Khalikuz Zaman, hatibu wa miskiti mkuu wa Chitral na maulamaa kadhaa wa Kipakistan walihudhuria kongamano hilo na kuzungumzia sira na maisha ya Mtume Muhammad (saw).
Walimtaja mtukufu huyo kuwa ni kigezo kamili kinachopaswa kuigwa na wanadamu wote na kusisitiza juu udharura wa kufuata misingi na kanuni za kimaadili za Nabii Muhammad (saw).
Kongamano hilo pia limetilia mkazo kwamba njia ya saada na ufanisi katika dunia hii na huko akhera ni kufuata sira na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw). Wanazuoni hao wa Kiislamu wamesisitiza kuwa hali inayotawala dunia ya sasa ni matokeo ya kupuuzwa mafundisho ya Nabii Muhammad (saw) na kutangaza kuwa migogoro na matatizo mengi ya dunia ya leo yatatatuliwa iwapo wanadamu watatekeleza ipasavyo mafundisho ya mtukufu huyo.
Kongamano hilo pia limehudhuriwa na wageni kutoka maeneo mbalimbali ya Pakistan. 718505