IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Wastani katika Uislamu' chamalizika Algeria

10:42 - December 27, 2010
Habari ID: 2053919
Kikao cha kimataifa cha 'Wastani katika Uislamu' kilimazika jana Jumapili huko Algiers, mji mkuu wa Algeria.
Kwa mujibu wa tovuti ya atlasinfo, kikao hicho cha siku mbili kilihudhuriwa na wanafikra pamoja na wasomi kutoka nchi kadhaa za Kiarabu.
Kikao hicho kilichofanyika chini ya anwani ya 'watsani na nafasi yake katika kulinda amani ya kijamii' kiliandaliwa na Jumuiya ya Mwongozo na Marekebisho ya Algeria kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wastani.
Washiriki walijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na athari nzuri za mielekeo na misimamo wastani katika jamii ya Algeria na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu.
Athari za misimamo hiyo katika maendeleo na ustawi wa nchi pamoja na athari za wanawake katika kuhuisha misimamo hiyo ni mambo mengine yaliyojadiliwa kwa kina katika kikao hicho cha Algeria. 718925
captcha