IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Makka kutangazwa redioni

14:00 - December 27, 2010
Habari ID: 2054193
Mashindano ya Kimataifa ya 32 ya Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia yameanza leo Jumatatu katika nyanja za hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur’ani Tukufu. Mashindno hayo yanayofanyika katika mji mtakatifu wa Makka yanarushwa hewani moja kwa moja kupitia Redio Qur’ani ya Saudia.
Mashindano hayo yanafanyika katika zamu mbili za asubuhi na alasiri huku majaji wa mashindano hayo wakitathmini na kuchunguza kiraa, hifdhi na tafsiri za washiriki.
Waziri wa Utamaduni na Habari wa Saudi Arabia Abdul Aziz bin Muhyiddin Khaujah amesema kuwa shughuli zote za mashindano hayo zinarushwa hewani kupitia Redio Qur’ani.
Amesisitiza kuwa kutangazwa mashindano hayo kwa njia ya moja kwa moja kuna taathira kubwa kwa Waislamu hususan tabaka la vijana ambao amewahimiza kufanya bidii katika kuhifadhi kitabu hicho kitukufu.
Vilevile Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislam ya America ya Latini Muhammad Yusuf Hajir amesema mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Saudi Arabia yanafanyika katika kiwango cha juu na kwamba zawadi zinazotolewa katika mashindano hayo zinawahamasisha vijana kutilia maanani kitabu hicho. 719071

captcha