Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Trad Mahmoud amesema, tawi hilo jipya linafunguliwa katika fremu ya kuimarisha huduma za Kiislamu kwa wateja.
Amesema tawi hilo jipya liko katika eneo la Al Kabaa mjini Sharja na ni tawi la 61 la benki hiyo katika maeneo mbalimbali ya Imarati.
Katika upande mwingine, Samah Ale Awadhullah Mkuu wa Benki ya Kiislamu ya Abu Dhabi amesema kuwa, lengo la kufunguliwa tawi jipya ni kupanua huduma za Kiislamu kwa wateja na kukidhi mahitaji yao ya kibenki pamoja na huduma bora.
Itakumbukwa kuwa Benki ya Kiislamu ya Abu Dhabi hivi karibuni iliteuliwa kuwa benki bora zaidi ya Kiislamu duniani.
719123