Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qatar QNA, nuskha hiyo ya Qur'ani imezawadiwa pembizoni mwa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani maalumu kwa wenye ulemavu wa macho nchini Qatar.
Katika mkutano wao, Al Kuwari na Al Naimy wamesisitiza kuhusu ushirikiano zaidi kwa lengo la kutambua matatizo ya wenye ulemavu wa macho na kutatua matatizo yao katika jamii. Aidha wametathmini jukumu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar kuhusu wenye ulemavu wa macho.
Jumapili tarehe 26 Disemba kituo cha waalimu wa Qur'ani cha Nur cha Qatar ambacho ni maalumu kwa wenye ulemavu wa macho kiliandaa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani katika viwango mbalimbali. Mashindano hayo yalifanyika katika kituo cha 'Arwa bint Abdul Muttalib' mjini Doha.
Mashindano hayo yamefanyika pembizoni mwa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Sheikh Ghanim bin Al Thani nchini Qatar. 719374