IQNA

Mashindano ya Qur'ani Lebanon

13:05 - December 28, 2010
Habari ID: 2054444
Duru ya 13 ya mashindano ya kila mwaka ya hifdhi, tilawa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu inaendelea nchini Lebanon.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano ya tafsiri ya sura "Yusuf" na "Maryam" yalifanyika Jumapili 26 Desemba katika miji mikubwa ya Lebanon ikiwa ni pamoja na mji mkuu Beirut na vile vile mjini Nabatiya na Sur.
Aidha Ijumaa tarehe 24 Desemba mashindano ya tafsiri ya sura hizo yalifanyika katika miji ya Balabak na Al Harmal.
Katika siku zijazo mashindano hayo yataingia katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika vitengo vya juzuu 5, juzuu 10, juzuu 20 na Qur'ani kamili na vilevile tilawa ya Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yana vitengo vya wanaume na wanawake.
719561

captcha