Wanazuoni, watafiti na wanafikra wa Kiislamu wanaoshiriki katika kikao hicho wamesisitiza pia umuhimu wa kuanzishwa vituo vya udhibiti na usimamiaji wa utekelezwaji wa masuala ya kisheria katika miamala ya kibiashara.
Kuwasilishwa mitazamo ya kifik'hi kuhusiana na masuala mapya yanayodhihiri katika maisha ya kila siku ya Waislamu yakiwemo ya kitiba, kiuchumi, kijamii na kifamilia, ni mambo mengine yanayojadiliwa katika kikao hicho kilichoanza siku ya Jumamosi.
Maulamaa na watafiti wa Kiislamu kutoka nchi kadhaa za Kiislamu wanashiriki katika kikao hicho ambacho kimepangwa kumalizika kesho Jumatano tarehe 29 Disemba. 719368