Gazeti la Al Ra’y la Jordan limeandika kuwa Banki ya Maendeleo ya Kiislamu IDB pamoja na Chuo cha Waqfu cha Islamia Cape Town ICCTT zimetiliana saini mkataba wa kugharamia chuo kipya cha waalimu mjini Cape Town Afrika Kusini.
Mkopo wa $ 350,000 wa IDP umetolewa wakati banki hiyo inajitahidi kuinua kiwango cha maendeleo na uelimishaji maulamaa wa Kiislamu kote duniani.
Akademia hiyo inatazamiwa kuwasaidia wanachuo wa Afrika katika utafiti, mafunzo na kufundisha lugha ya Kiarabu ili kustawisha masomo ya Kiislamu kusini mwa Afrika.
720051