Madrasa ya wanawake ya mafunzo ya Qur'ani ya Dar as-Sumuw ya Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, imechaguliwa kuwa madarasa na kituo bora zaidi cha mafundisho ya Qur'ani katika mwaka uliopita wa Hijria wa 1431.
Madrasa hiyo ya wanawake iliibuka kuwa ya kwanza mwaka huo katika mafundisho ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Muhammad bin Ahmad as-Shimri, mkuu wa madrasa hiyo amefurahishwa na ushindi huo na kusema kuwa unatokana na juhudi kubwa zinazofanywa na madrasa hiyo katika kuimarisha uhusiano wake na vituo vya mafunzo ya Qur'ani katika mji wa Riyadh.
Ameishukuru Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Hifdhi ya Qur'ani ya Riyadh kutokana na msaada wake wa kimaada na kimaanawi katika kufanikisha shughuli za madrasa hiyo kwa lengo la kuhudumia kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Madrasa ya Dar as-Sumuw hutoa mafunzo mepesi ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu pamoja na tafsiri na sheria za Kiislamu kwa wanawake wenye umri tofauti. Pia hutoa masomo ya mbinu za kuhifadhi Qur'ani na utoaji hutuba kwa wanafunzi wake. 721036