IQNA

Kikao cha kimataifa cha Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu mjini Cairo

11:50 - December 30, 2010
Habari ID: 2055860
Kikao cha Kimataifa cha Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu kimepangwa kufanyika tarehe 10 hadi 13 Februari huko Cairo mji mkuu wa Misri.
Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na Quds Tukufu katika historia, Quds katika dini za mbinguni, Quds katika utamaduni wa Kiislamu, kudhibitiwa Quds na sheria za kimataifa na hali ya hivi sasa na ya baadaye ya Quds.
Kamati inayoandaa kikao hicho imewaalika mawaziri wa wakfu na masuala ya Kiislamu pamoja na mamufti wa nchi za Kiislamu, maulamaa, wanafikra na wataalamu wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za dunia kushiriki katika kikao hicho.
Mazungumzo ya meza-duara ya kujadili mazungumzo kati ya tamaduni na dini tofauti pia yamepangwa kufanyika pambizoni mwa kikao hicho.
Wasoni 20 walio na ujuzi kuhusiana na suala la mazungumzo kati ya staarabu na dini tofauti kutoka nchi za Ulaya na Marekani wamealikwa pia kushiriki katika mazungumzo hayo.
Kikao hicho ambacho kitafanyika kwa uungaji mkono wa Rais Hosni Mubarak wa Misri tayari kimekwishatuma barua za mwaliko kwa mamufti, mawaziri wa wakfu, wanafikra na watafiti wa Kiislamu 180 ili kushiriki katika kikao hicho. 721010
captcha