IQNA

Idhaa ya Kiislamu ya Nur yazinduliwa Cameroon

12:38 - January 01, 2011
Habari ID: 2056408
Idhaa ya Kiislamu ya Nur ilizinduliwa jana Ijumaa huko katika mkoa wa Adamaoua nchini Cameroon.
Kwa mujibu wa tovuti ya journalducameroun, shakhsia mbalimbali wa Kiislamu, Mkuu wa Mkoa wa Adamaoua na wapenzi wa masuala ya kidini ni miongoni mwa wageni waalikwa walioshiriki katika ufunguzi wa idhaa hiyo.
Lengo la kuzinduliwa idhaa hiyo ni kutangaza vipindi mbalimbali vya kuvutia katika nyanja za dini na utamaduni yakiwemo mafunzo ya kaligrafia na usomaji Qur'ani Tukufu pamoja na hotuba za wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu. Matangazo hayo yatakuwa yakirushwa hewani kwa lugha za Kiarabu na Kifulani.
Huku wakisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika ulimwengu za sasa, wanazuoni na maafisa wa serikali waliohudhuria kikao cha uzinduzi wa idhaa hiyo walisema kuwa huo ni mwanzo na hatua muhimu katika juhudi za kuimarisha thamani za kidini na kimaanawi katika jamii ya Cameroon.
Inasemekana kuwa jumuiya ya kidini ya Wito wa Kiislamu nchini Cameroon ndiyo inayodhamini gharama za idhaa hiyo. 721678
captcha