Kituo cha Habari cha The Record kimeripoti kuwa mbali na kutoa ombi hilo kwa Jumuiya ya Shule za eneo hilo, Kituo cha Habari cha Kiislamu cha Waterloo kimetangaza kuwa iwapo ombi hilo litakubaliwa kitatoa nakala ya Qur'ani Tukufu kwa kila mwanafunzi wa darasa la tano katika mwaka wa masomo wa 2011-2012.
Hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuwaelimisha wanafunzi na familia zao kitabu kitakatifu cha Qur'ani kupitia tarjumi ya Kiingereza ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. 722211